Propellerads

Ona hii, Wenger awalinganisha Sanchez na Suarez na ametoa matazamo wake



Kocha Arsene Wenger amesema kua mchezaji wake
Alexis Sanchez analingana kiuwezo na Luis Suarez wa Barcelona.

Barca walimuuza Sanchez kwa Wenger kiasi cha £35m  majira yaliyopita ya joto, ambapo kwa kuziba pengo wakali hao wa Catalan wakamnunua Suarez kutoka Liverpool kwa ada ya  £70m

Mwaka 2013 Wenger aliweka dau kumchukua Suarez, lakini hata hivyo dau hilo lilikataliwa. Sasa Wenger anasema ana furaha alifanikiwa kumpata Sanchez badala yake, na hana wasi wasi kwani wachezaji hao wote wawili wana viwango sawa

"Sanchez na Suarez wako level moja, Suarez ni mshambuliaji wa kati, Sanchez ni mchezaji anayepanda na kushuka, lakini wnafanana" aliwaambia maripota.

"Sanchez hua anakua na ukame wa kufunga, kuleta hatari kwa mabeki, kwa sababu anaweza kukatiza katikati yao sio pembeni na kuwakimbiza"

"Sanchez hucheza kushinda kila mechi, niliwahi kua na wachezaji kama yeye, ambao wanataka sana kushinda"

Arsenal watawakaribisha Liverpool uwanja wa Emirates Jumatatu hii usiku.


Ona hii, Wenger awalinganisha Sanchez na Suarez na ametoa matazamo wake Ona hii, Wenger awalinganisha Sanchez na Suarez na ametoa matazamo wake Reviewed by Steve on Sunday, August 23, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.