Wenger ammwagia sifa Sanchez baada ya ushindi wa jana
Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger amemmwagia sifa mchezaji
wake Alexis Sanchez kwa moyo wa kujituma aliouonesha kutika mechi waliyoshinda 2-1 dhidi ya Crystal Palace ilhali hayuko fit kivile baada ya majeraha.
Tambo za Mourinho baada ya kipigo cha Man City,
Sanchez alirejea kwenye nafasi yake jana na kucheza dakika 75 ikiwa ni mechi yake ya kwanza msimu huu baada ya mechi za kimataifa, ambapo alionesha tofauti kubwa kwani alichangia bao la ushidi kwa Arsenal lile la kujifunga la Damien Delaney wa Crystal Palace.
"Kupiga kile kichwa haikua kama bahati, ni kama vile alifunga Sanchez akiwa na ukame" alisema Wenger kwa mujibu wa FourFourTwo.com
"Bado hajawa fit kidogo, lakini ni mpambanaji"
Kikosi cha Wenger sasa kina pointi tatu katika meche mbili baada ya kupoteza mechi ya kwanza dhidi ya West Ham.
Wenger ammwagia sifa Sanchez baada ya ushindi wa jana
Reviewed by Steve
on
Monday, August 17, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Monday, August 17, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment