Propellerads

Ona jinsi Mourinho alivyoubeza ushindi wa Man City, ameuita jina hili




Mourinho ameubeza ushindi wa 3-0 walioupata Man City jana dhidi
ya Chelsea ambapo ameuita kua ni 'ushindi feki'.

Sergio Aguero ndie aliefungua karamu ya magoli kwa City ndani ya dakika 45 za kipindi cha mwanzo, kabla ya kina Vincent Kompany na Fernandinho waliofunga katika kipindi cha pili.

Hata hivyo Mourinho ambaye timu yake ilipiga mashuti matatu pekee kwenye target, amedai The Blues walifanya vizuri zaidi kipindi cha pili.

"Timu nzuri kipindi cha kwanza ilishinda mchezo,. Timu nzuri kipindi cha pili kwa hakika ilikua ni Chelsea" aliiambia Sky Sports News

"Kipindi cha kwanza kilikua kigumu, hatukutengeneza nafasi nyingi na golikipa wetu aliokoa mara chache. Kipindi cha pili mambo yalikua tofauti.

"Ushindi wa 1-0 haukua na shaka yoyote mpaka dakika ya 70, 3-0 ni feki kabisa. Kwa 1-0 Chelsea ilikua ni bora zaidi kipindi chote cha pili"

Kipigo hicho kimewaacha Chelsea nyuma ya pointi tano kwa Man City.

Ona jinsi Mourinho alivyoubeza ushindi wa Man City, ameuita jina hili Ona jinsi Mourinho alivyoubeza ushindi wa Man City, ameuita jina hili Reviewed by Steve on Monday, August 17, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.