Propellerads

Tambo za Mourinho baada ya kipigo cha Man City,



Kocha Jose Mourinho ametamba kua bado wana uwezo wa kuchukua ubingwa
msimu huu bila kujali kipigo cha 3-0 jana kutoka kwa Man City.

Man City imekua kwmwa wanatoa onyo mapema juu ya ubingwa kufuatia Sergio Aguero, Vincent Kompany na Fernandinho kuwanyamazisha mabingwa hao pale Etihad.

Sare na Swansea katika mechi yao ya kwanza wiki iliyopita, kipigo hiki kimemwacha Mourinho na kikosi chake wakiwa na pointi moja tu mkononi, huku Mourinho akidai ni mapema sana kuzungumzia swala la ubingwa.

"Pointi moja badala ya sita ni bora zaidi kuliko kukosa kabisa na ni mbaya zaidi ingekua mechi zaidi ya mbili" Mourinho aliiambia Sky Sports.

"Niko vizuri katika hesabu. Ukizidisha 36 kwa tatu najua unapata ngapi, najua ubingwa ni zaidi ya hesabu za wazi"

Katika mchezo unaofata jumapili ijayo, Chelsea watasafiri kuwakabili  West Bromwich Albion huku wakiwa na matumaini ya kupata ubingwa wa kwanza.
Tambo za Mourinho baada ya kipigo cha Man City, Tambo za Mourinho baada ya kipigo cha Man City, Reviewed by Steve on Monday, August 17, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.