Propellerads

Washindi wa bahati nasibu Simba day wapewa zawadi leo, shuhudia baadhi ya picha

                                         Ahazi Mwembe (kushoto) akikabidhiwa zawadi yake na Rais wa Simba Evans Aveva

Uongozi wa klabu ya Simba leo umetoa zawadi kwa washindi wa bahati na sibu iliyochezeshwa siku ya
Simba Day Aosti 8 mwaka huu wakati wa kilele cha sherehe za siku ya Simba Day zilizofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Cheki Yanga wakikomaa na tizi Tukuyu



Zawadi zilizo kabidhiwa kwa washindi ni jezi pamoja simu, kila mshindi amepata jezi ya juu pea moja pamoja na simu moja aina ya Motec. Washindi wa zawadi hizo ni Jeremia Venist, Ahazi Mwembe pamoja na Marko Mgimba.

Washindi wa bahatinasibu (kutoka kushoto ni Jeremia Venist, Ahazi Mwembe na Marko Mgimba) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao

 Mbali na zawadi hizo, klabu hiyo pia imekabidhi mipira nane kwa shule mbili za msingi za mkoa wa Dar es Salaam ambapo Shule ya Msingi Mikocheni A imepata mipira minne huku Shule ya Mingi Chang’ombe Mazoezi nayo ikikabidhiwa mipira minne.

Rais wa Simba Evans Aveva akimkabidhi mpira mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mikocheni A

Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva amesema, klabu hiyo inataka kusaidia soka la vijana nchini na kwasasa wameanza na mkoa wa Dar es Salaam lakini baadae watasonga mbele hadi kwenye mikoa mingine ili kuwafikia watu wengi zaidi hasa watoto ambapo ndio leno hasa la klabu hiyo kusaidia soka la vijana.

Mwandishi mwandamizi wa mtandao wa Shaffihdauda.com Dickson Masanja (kushoto) akipokea mpira kutoka kwa Rais wa Simba baada ya kushinda bahatinasibu iliyochezeshwa ikishirikisha wanahabari

Washindi wa bahati nasibu Simba day wapewa zawadi leo, shuhudia baadhi ya picha Washindi wa bahati nasibu Simba day wapewa zawadi leo, shuhudia baadhi ya picha Reviewed by Steve on Thursday, August 13, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.