Propellerads

Usajili Ulaya, mapya yaliyojiri leo





Harakati za usajili bado zinaendelea Ulaya kwa sasa, leo nakuletea
mapya ambaye yamejiri katika uhamisho wa nyota mbali mbali nikiangazia kina Sergio Ramos, Baba Rahman, Xerdan Shaqiri, Kevin De Bruyne, Harry Kane na Alexandre Lacazette.

Possible line ups Barca na Sevilla leo jumanne, Pedro yumo!!

Ramos kusaini dili jipya wiki hii
Kulingana na ripoti kutoka Hispania, Ramos atasaini mkataba mpya na Real Madrid alhamisi hii, hivyo kuzima uvumi wa kuhamia Man United.

Chelsea kumalizana na nyota wa kiafrika
Chelsea wameripotiwa kua katika hatua za mwisho kumsainisha Baba Rahman kwa dili litakalogharimu pauni 25m hivyo kuziba pengo la beki wa kushoto lililoachwa na Luis Fellipe.

Shaqiri amechukua vipimo vya afya Stoke
Aliyekua winga wa Bayern Munich, Xerdan Shaqiri yuko katika hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wake kuingia Stoke City, kwani inadaiwa tayari amechukua vipimo vya afya jana Jumatatu.

City mbioni kukamilisha dili la De Bruyne
Inadaiwa kua Man City wana imani kubwa ya kumnasa nyota wa Wolfsburg, Kelvin De Bruyne kabla hata ya Jumamosi kwenye mechi dhidi ya Chelsea, dau waliloweka inasemekana ni pauni 40m, huku Wolfsburg wao wanataka pauni 50m, lakini City wameripotiwa kuweka dau hilo pekee  na kama wakiongeza ni pauni 6m pekee hivyo kufikia pauni 46m.

Man Utd kumtolea Kane ofa ya pauni 40m?
Man United wanataka kumnasa nyota wa Tottenham ,Harry Kane kwa dau la pauni 40m. Mara kadhaa kocha Louis van Gaal amekaririwa akisema timu bado inahitaji mshambuliaji, hivyo iko wazi Red Devils wanajiandaa kumnasa Kane.

Cheki picha Man City alivyoua jana

West Brom kufanya usajili wenye kuvunja rekodi
West Bromwich wamethibitisha kumsajili Salomon Rondon kutoka Zenit St. Petersburg kwa usajili uliovunja rekodi ndani ya klabu hiyo.

Kwingineko
Nyota aliyekua akiwaniwa na Arsenal na Man United, Alexandre Lacazette  amesaini mkataba wa miaka minne na Lyon.

Usajili Ulaya, mapya yaliyojiri leo Usajili Ulaya, mapya yaliyojiri leo Reviewed by Steve on Tuesday, August 11, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.