Propellerads

Nini hatma ya mshambuliaji huyu wa Simba??!!, mwenyewe abaki njia panda




Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Elius Maguri amesema hadi sasa hajajua
sababu rasmi ya kuachwa na wekundu hao wa Msimbazi.
Kwa mujibu wa Maguri,  amekuwa akituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa viongozi wa Klabu hiyo ikiwa ni pamoja na kuwapigia simu kutaka kujua hatma yake, lakini hapati majibu.
Maguri amefafanua kwamba walipotoka Zanzibar ambako waliweka kambi ya wiki mbili, wachezaji walitakiwa kuingia kambini kujiandaa na mechi ya Simba Day dhidi ya Sports Club Villa ya Uganda, lakini jina lake halikuwepo kwenye orodha ya wachezaji waliotakiwa kuingia kambini.
Taarifa za chini zinaeleza kwamba, Simba inataka kumtoa kwa mkopo au kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja kwasababu hayupo kwenye mipango ya kocha Dylan Kerr.
Nini hatma ya mshambuliaji huyu wa Simba??!!, mwenyewe abaki njia panda Nini hatma ya mshambuliaji huyu wa Simba??!!, mwenyewe abaki njia panda Reviewed by Steve on Tuesday, August 11, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.