Propellerads

Uhamisho wa De Gea: Van Gaal avilaumu vyombo vya habari




Kocha wa Man United, Louis van Gaal amevitupia lawama
vyombo vya habari juu ya swala la uhamisho wa De Gea.

Van Gaal alikuana mkutano na waandishi wa habari juu ya mechi ya leo usiku dhidi ya FC Brugge ambapo amefunguka kuhusu uhamisho wa kipa huyo.

Alipoulizwa swali kua anaonaje kama Juan Mata acheze kati zaidi kumsaidia Wayne Rooney, alijibu kwa ghadhabu.

           
"Labda uiulize bodi ya Manchester United kama wewe ni mkufunzi wa kocha wa Manchester United" aliwaambia waandishi.

"Kila nikisema kitu vyombo vya habari vinaweka katika maana nyingine, nimeliona hilo katika suala la De Gea"

Van Gaal alimshambulia mmoja ya waandishi aliyeuliza kama Rooney ni mshambuliaji aliyestahili kumaliza ligi na magoli 20 huku kiwango chake kikionekana kushuka hasa katika michezo miwili ya mwanzo msimu huu.

"Vyombo vya habari vimeandika mwaka mzima kua nimweke kua mshambuliaji, inashangaza kuona baada ya michezo miwili unaanza kuweka mashaka kwa maoni yako. Nashindwa kuelewa hii"

"Ninajiamini kwa wachezaji wangu" aqlimaliza.

Man United wanaumana na FC Brugges ya Ubelgiji leo usiku katika michuano ya klabu bingwa, na kama wakishinda wataendelea katika hatua ya makundi.
Uhamisho wa De Gea: Van Gaal avilaumu vyombo vya habari Uhamisho wa De Gea: Van Gaal avilaumu vyombo vya habari Reviewed by Steve on Tuesday, August 18, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.