Propellerads

Chelsea kuvunja rekodi kwa Stones, pia wanamfukuzia mwingine



CHELSEA wanatarajiwa kuweka rekodi ya uhamisho kwa
kuweka dau jipya la John Stones ambaye tayari ofa mbili za mwanzo zilikataliwa na Everton.

Bodi ya klabu ya Chelsea imeamua kuchukua maamuzi kufuatia kipigo cha magoli 3-0 kutoka kwa Man City jumapili iliyopita, pia kitendo cha kutolewa John Terry- maamuzi hayo ni kuongeza ofa nyingine ili kumnasa beki huyo, jambo

Hii ni ofa ya tatu kwa kocha Jose Mourinho kwa Everton baada ya ofa ya £20m kisha £26m zote kukataliwa.

Usajili wa Man City kwa  Eliaquim Mangala wa pauni 32m majira yaliyopita ulimfanya beki huyo kua ghali zaidi katika historia Premier League, lakini dili hili la John Stones ndio litakaloweka rekodi ya kua ghali zaidi.

Inasemeka katika kipindi hiki cha siku 15 za usajili zilizobaki, mmiliki wa klabu, Roman Abramovich amekusudia kuongeza nguvu ili kuoendelea kua katika mbio za kutetea ubingwa wao wa ligi.
Mourinho ambaye wiki iliyopita alikosana karibia na kila mtu, pia anajipanga kumnasa Alexandre Lacazette kwa dau la  £21m.



Chelsea kuvunja rekodi kwa Stones, pia wanamfukuzia mwingine Chelsea kuvunja rekodi kwa Stones, pia wanamfukuzia mwingine Reviewed by Steve on Tuesday, August 18, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.