Propellerads

Uhamisho Benzema na Pedro unazidi kua mgumu, klabu nyingine tena yaibukia dili




Wakati Manchester United wako katika juhudi kuu kuhakikisha
wanambasa Pedro Rodriguez wa Barcelona, wapinzani wao wakubwa Manchester City nao wameingia vitani.

Man City wameingia vitani wakitaka kumpata nyota huyo huku kukiwa na taarifa nyingine pia wanamhitaji Karim Benzema ambaye anatakiwa na Arsenal.

Tayari Pedro amesema anaweza kuondoka Barcelona kwa kuwa inaonekana haelewani na Kocha Louis Enrique lakini uamuzi wa City kuanza kumfuatilia unaamsha vita mpya kabisa.

Tayari Man United iko tayari kutoa pauni milioni 22 kumpata, kuingia kwa City kunaweza kusababisha kupanda kwa bei ya kiungo huyo mwenye miaka 28.

Man United inataka kumchukua kwa lengo kuziba nafasi ya Angel Di Maria ambaye amekwenda PSG.

Pedro ndiye alikuwa shujaa wa Barcelona baada ya kufunga bao lililoipa Barcelona ubingwa wa Uefa Super Cup kwa kuichapa Sevilla kwa mabao 5-4.
Uhamisho Benzema na Pedro unazidi kua mgumu, klabu nyingine tena yaibukia dili Uhamisho Benzema na Pedro unazidi kua mgumu, klabu nyingine tena yaibukia dili Reviewed by Steve on Thursday, August 13, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.