Pluijm ameongea yake baada ya mchezo wa jana na Prisons
Pamoja na kuichapa Prisons kwa mabao 2-0 jana, Kocha
Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema kuna mambo kadhaa ya kurekebisha.
Pluijm amesema anataka kurekebisha mambo mengi ambayo ameyaona katika mechi mbili za kirafiki kwa kuwa viwanja vya mikoani pia hutoa taswira nzuri.
“Viwanja vingi vya mikoani si vizuri, mnapocheza mechi utaona tofauti kubwa na mnapocheza Dar es Salaam.
“Hivyo bado kuna mambo kadhaa ya kurekebisha, tutaendelea kufanya na kwa kuwa tutacheza na Mbeya City kwenye uwanja huo, tutakuwa na nafasi ya kuyafanyia kazi tena ambayo tumerekebisha,” alisema Pluijm.
Yanga tayari imecheza mechi mbili, ikianza na Kimondo mjini Mbozi na kuifunga mabao 4-1 kabla ya kuichachafya Prisons kwa mabao 2-0.
Pluijm ameongea yake baada ya mchezo wa jana na Prisons
Reviewed by Steve
on
Thursday, August 13, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, August 13, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment