Di Maria ametaja wakali hawa wanne anaowakubali
Winga muarjentina, Angel Di Maria ametaja nyota
wanne kutoka katika klabu yake ya sasa ya PSG ambao anatarajia kujifunza mengi kutoka kwao msimu huu.
Nyota huyo ambaye hivi karibuni alikamilisha uhamisho wake wa Euro 63mil akitokea Man United, amepata kucheza na baadhi ya nyota wakubwa ulimwenguni na sasa kutua kwake PSG kunaweza kuongeza kitu kingine katika CV yake.
Akiongea na vyombo vya habari, amesema atajifunza zaidi kwa akina Ibrahimovic, Thiago Silva
"Mtuunajifunza kila siku, kwa viwango vya wachezaji kama Zlatan Ibrahimovic, Marco Verratti, Thiago Silva, Edinson Cavani na wengine wengi, nadhani naenda kujifunza mengi" aliiambia website rasmi ya PSG.
"Naelekea kuendelea kukua, bado kijana. Mchezaji anajifunza mpaka mwisho wa kazi yake., msimu baada ya msimu. Nitajitahidi kutumia nafasi ya kua karibu na nyota hawa"
Di Maria amepata kuchezea vilabu vikubwa kama vile Benfica, Real Madrid na Man United, uhamisho wa PSG ni hatua nyingine kubwa kwake.
Di Maria ametaja wakali hawa wanne anaowakubali
Reviewed by Steve
on
Thursday, August 13, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, August 13, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment