Propellerads

Kauli ya Messi kuhusu suala la uhamisho wa Pedro.




Nyota wa FC Barcelona, Lionel Messi ametoa maoni yake kuhusu
hatma ya Pedro ambaye ameripotiwa kutaka kuhamia Barcelona.

Pedro  alifunga kwenye muda wa nyongeza goli la ushindi wa 5-4 dhidi ya Sevilla kwenye fainali ya Super Cup jumanne lakini hata hivyo alionekana kutokua na furaha wakati wenzake wakisharehekea ubingwa huo.

Messi amezungumzia hali ya Pedro na kusema alistahili kufunga kwenye mechi hiyo.

"Alistahili kwa kila kitu alichofanya na pia kuendelea kuwepo klabuni"

"Sijui nini kitatokea kwake, anatakiwa afanye maamuzi, lakini kila anachofanya kinamstahili"

Pedro alilalamika kwanini alianzia benchi huku Neymar hakuepo.

Hata hivyo mkurugenzi wa sasa wa michezo wa Barca, Robert Fernandez anadai Pedro alimwambia anataka kuondoka klabuni ndio sababu iliyopelekea akaanziia benchi.

Nae kocha Luis Enrique anasema kua Pedro alipata majeraha kidogo siku mbili kabla ya mechi hiyo kwa hiyo akawa substitute kama tahadhari na si vinginevyo.


Kauli ya Messi kuhusu suala la uhamisho wa Pedro. Kauli ya Messi kuhusu suala la uhamisho wa Pedro. Reviewed by Steve on Thursday, August 13, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.