Inawezekana kweli van Gaal hapendi wabrazil!!...soma madai ya Rafael
Nyota mpya wa Lyon, Rafael ambaye alisaini akitokea Man United, amedai
kua kocha wa Red Devils, Louis van Gaal alikua anaharibu kipaji chake na hakumpenda.
Kuhusu uvumi wa kua van Gaal hapendi wachezaji wa kibrazil beki huyo amesema kua hawezi kuchangia chochote, lakini anadai bosi huyo hakumpenda kama mchezaji wa timu huku akikazia kua kuondoka kwa Ferguson lilikua ni pigo kubwa katika kipaji chake.
"Sijui kwa kweli. Siwezi kulizungumzia hilo, kwa sababu nilikua peke yangu tangu Anderson alipoondoka" aliiambia Globo Esporte.
"Naijua hii stori kua hapendi wabrazil, lakini siwezi kusema 'ooh hapendi wabrazil'.
"Najua kua hanipendi mimi, kama sababu mimi ni mbrazil, sijui"
Rafael ameeleza kua kipindi cha Ferguson mambo yalikua mazuri kwake, lakini kuwasili kwa kocha van Gaal hali ilibadilika.
"Nilicheza msimu mzima, Ferguson alipoondoka. Kipindi cha 2012-13 nilicheza karibu kila mchezo , ulikua ni msimu mzuri sana kwangu, na tulikua mabingwa"
"Kwa van Gaal uhusiano ulikua kawaida, kila kocha ana mawazo yake na mtazamo wake"
"Meneja ni meneja tu, namheshimu na siku zote nitamheshimu"
Inawezekana kweli van Gaal hapendi wabrazil!!...soma madai ya Rafael
Reviewed by Steve
on
Wednesday, August 12, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Wednesday, August 12, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment