Ripoti:Huku Cuadrado akitua Juve, Chelsea kuvunja rekodi kwa Pogba!!
Chelsea wanajipanga kuvunja rekodi yao ya usajili
kwa Pogba kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili,
Nyota huyo mfaransa aliripotiwa sana kuwindwa na vilabu vya Barcelona na Man City, lakini walishindwa kufikia ofa iliyotakiwa na Juve.
Hata hivyo the London Evening Standard wameripoti kua Mourinho anajipanga kutumia kiasi zaidi ya pauni 50m ambayo alitumia kumleta Torres mwaka 2011.
Hii inakuja baada ya jana mchezaji wa Chelsea Juan Cuadrado kutua Italia tayari kukamilisha mipango ya uhamisho wake Juve. Ikumbukwe Cuadrado alikua anataka kutumiwa na Mourinho kama sehemu ya dili la kumpata Pogba.
Kwa sasa Pogba ana thamani inayotajwa kufikia £71m.
Ripoti:Huku Cuadrado akitua Juve, Chelsea kuvunja rekodi kwa Pogba!!
Reviewed by Steve
on
Tuesday, August 25, 2015
Rating:

No comments:
Post a Comment