Propellerads

Pedro aeleza kumbe sio Man United tu hata Man City walimtaka!!



Nyota mpya wa Chelsea Pedro amefichua mambo kua ukiachilia
mbali Man United pia Man City nao walikua wakimfukuzia.

Mchezaji huyo alikua akihusishwa kwa muda mrefu na Manchester United kabla hajafanya uhamisho wa kushtukiza na kutua Chelsea wiki iliyopita.

Japokua kocha Louis van Gaal amekua akikanusha kua hakutaka kumsajili, Pedro mwenyewe ameweka wazi Red Devils waliitaka saini yake.

Ameyasema hayo wakati akiwa kwenye mkutano na waandishi jijini Barcelona alikokua amerudi kuaga rasmi.

"Nilipata sana ushawishi kutoka vilabu vikubwa vya England, United, City na Chelsea " AS walimnukuu Pedro  "Ofa ya Chelsea ndio iliyonishawishi zaidi"

Winger huyo aliifungia Chelsea kwenye mechi dhidi ya West Brom jumapili ambapo walishinda 3-2.
Pedro aeleza kumbe sio Man United tu hata Man City walimtaka!! Pedro aeleza kumbe sio Man United tu hata Man City walimtaka!! Reviewed by Steve on Tuesday, August 25, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.