Muller 'apuuza' uvumi unaoendelea kuhusu swala lake la uhamisho, je ni kweli anataka Manchester?
Nyota wa Bayern Munich, Thomas Muller amefunguka na kudai kua
yeye hajali sana tetesi zinazoendelea sasa katika vyombo mbali mbali vya habari kwamba anataka kuhamia Manchester United.
Taarifa zilizopo sasa zinadai Red Devils wapo tayari kutoa ofa ya £71m ili kuipata saini ya nyota huyo.
Hata hivyo, Muller ambaye amewahi kufanya kazi na kocha Louis van Gaal klabuni Bayern, amekanusha taarifa hizo na kusema kua tetesi hua ni sehemu ya maisha kwa wachezaji wakubwa.
"Ni upuuzi, mambo ya sasa yanayoongelewa katika soka" aliongea katika kipindi cha televisheni kiitwacho Bundesliga Aktuell.
"Hii ndio hali halisi ya hii biashara, kwa hiyo sina wasi wasi"
"Nilipokua Dressden, shabiki mmoja alinifuata akiwa na kipaza sauti akasema, Hey bwana Mr €100 million, jezi yako ina thamani gani?..nilitabasamu tu
Mkataba wa sasa wa Muller ni mpaka 2019 katika klabu hiyo ya Allianz Arena.
Muller 'apuuza' uvumi unaoendelea kuhusu swala lake la uhamisho, je ni kweli anataka Manchester?
Reviewed by Steve
on
Friday, August 21, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, August 21, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment