Chelsea kutumia tena pesa za kutosha kuwanasa Stones, Pogba
Chelsea wanatarajiwa kutumia kiasi kikubwa cha pesa kitakachofikia
£120m kuwanasa John Stones na Paul Pogba.
Wiki hii klabu hiyo iliwashangaza Man United kwa kumsajili Pedro kwa kiasi cha £21.4m wakati wao wakiwa wakiwa hatua za mwishoni, na kwa sasa inadaiwa kua Mourinho anataka kutumia kiasi kinachokaribia £200m kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili September tarehe 1.
Chelsea wanajiandaa kumtengea ofa nyingine ambayo itakua ya nne inayofikia £40m beki wa John Stones wa Everton ndani ya masaa 48 yajayo. Pia Mourinho bado anaonesha nia ya kumhitaji Paul Pogba ambapo anadaiwa kutaka kumtumia Juan Cuadrado kama sehemu ya dili hilo.
Cuadrado tayari ana maongezi na Juventus juu ya mkopo wa muda mrefu na pia uwezekano wa mkataba wa kudumu msimu unaofatia.
Lakini pia Oscar anaweza kua ndani ya mpango huu pia kwani Juventus walimwekea ofa ya £26m ambayo ilikataliwa na Chelsea, kwa kuwatumia Cuadrado au Oscar, Chelsea inaweza kukamilisha mpango wake huo wa kumleta Pogba darajani.
Chelsea kutumia tena pesa za kutosha kuwanasa Stones, Pogba
Reviewed by Steve
on
Friday, August 21, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, August 21, 2015
Rating:




No comments:
Post a Comment