Propellerads

Kumbe ilikua Mavugo ajiunge Simba, nini kikatokea??!..mwenyewe aongea




Mshambuliaji Laudit Mavugo amesema alikuwa tayari kujiunga Simba kwa
moyo safi lakini kutoelewana kwa viongozi wa pande mbili, ndiyo kumesababisha.

Akizungumza na mtandao mmoja maarufu, Mavugo amesema kulitokea tofauti ndogo ndogo sana kati ya viongozi wa timu yake ya Vital’O na Simba.

Amesema alishamalizana na Simba kwa maana ya makubaliano, ndiyo maana alichukua hadi baadhi ya fedha lakini waliposhindana wenyewe, hakuwa na ujanja.

“Kitu cha kwanza kilikuwa ni kuhusiana na fedha wanazodai kuhusiana na uhamisho wa Amissi Tambwe ambazo hawajalipwa hadi leo.

“Pili viongozi wa Vital’O waliona Simba kama hawana ushirikiano na wana dharau, hmaana waliwaomba mechi ya kirafiki, hawakujibu wala kujali lolote,” alisema Mavugo.
Kumbe ilikua Mavugo ajiunge Simba, nini kikatokea??!..mwenyewe aongea Kumbe ilikua Mavugo ajiunge Simba, nini kikatokea??!..mwenyewe aongea Reviewed by Steve on Monday, August 10, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.