Propellerads

Hatimaye Mourinho awalegezea madaktari wa timu




Kwa wiki hii ukiachana na habari ya nani kamfunga nani kwenye EPL basi habari ya
Dr Eva iliandikwa sana na vyombo vya habari. Kama ilikupita ni kwamba Dr Eva alimkasirisha manager Jose Mourinho baada ya kuingia uwanjani kwenda kumtibia mchezaji Hazard dakika za lala salama wakati Chelsea ikiwa na wachezaji wachache uwanjani.

Muda mchache uliopita kwenye mkutano na waandishi wa habari Jose amesema kwamba yeye ana uhusiano mzuri na timu yake nzuri ya matibabu ambayo inaongozwa na Dr Paco Biosca.

Wameniambia kwamba hawajawai kusifiwa kwa kazi nzuri kama ilivyokua kwa miaka michache iliyopita walivyofanya kazi na mimi.

Pia maneno ambayo yameonekana kulegeza tatizo ambalo limetokea kati yake na Dr wa uwanjani, Mourinho amesema Dr Jon na Carneiro hawatakua kwenye benchi Jumapili hii. Lakini kutokua kwenye benchi haimaanishi kwamba hawatarudi tena kwenye benchi hilo. Hivyo basi hapo baadae tunaweza kuwaona tena kwenye benchi hilo la Chelsea.
Hatimaye Mourinho awalegezea madaktari wa timu Hatimaye Mourinho awalegezea madaktari wa timu Reviewed by Steve on Friday, August 14, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.