Van Gaal ameongea kuhusu kiwango cha timu yake baada ya mechi na Aston Villa
Louis van Gaal ameeleza kua ana furaha kutokana na mwanzo
mzuri wa Manchester United baada ya kushinda mechi ya jana dhidi ya Aston Villa ambapo walishinda 1-0
Red Devils wamepata kupiga mashuti matatu pekee yaliyolenga goli katika michezo yote miwili ya mwanzo, lakini juhudi zote hizo zimefanikisha kupata pointi sita.
Hata hivyo, pamoja na kawaida ya kupata upinzani mkali kila wakikutana na Tottenham au Aston Villa, Van Gaal amedai Man United sasa wako bora zaidi kuliko mwanzo wa msimu uliopita.
"Mwanzo wa msimu huu ni bora zaidi kuliko ule wa msimu uliopita lakini sio mgumu sana. Tulikua na point moja katika hatua hii na sasa tuna sita, kwa hiyo nina furaha" aliiambia Sky Sports
"Bada tuna safari ndefu, huwezi kuitabiri kwenye wiki nne tu za mwanzo. Tunahitaji mechi zaidi tuwe sawa, nadhani tunaweza kufanya hivyo". Alimaliza.
Goli la pekee la Man United lilipata kufungwa na nyota mbelgiji, Adnan Januzaj.
Van Gaal ameongea kuhusu kiwango cha timu yake baada ya mechi na Aston Villa
Reviewed by Steve
on
Saturday, August 15, 2015
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, August 15, 2015
Rating:










No comments:
Post a Comment