Propellerads

Chelsea nao wanataka kuingilia dili la Pedro?!!



Chelsea nao wanadaiwa kutaka kumnasa na wanajiandaa kuweka ofa kwa
nyota Pedro wa Barcelona ambaye pia tayari klabu ya Manchester United walishaanza harakati za kumpata.

Matukio katika picha, Man United alivyoua jana usiku!

Lakini hata hivyo Man United bado wako katika nafasi kubwa ya kumnasa nyota huyo, kwani kiongozi mmoja wa juu wa Man Uited, Ed Woodward jana jumatatu aliripotiwa kuelekea Barcelona kukamilisha dili hilo.

Taarifa hizi mpya zimekuja kufuatia klabu ya Chelsea kutaka kuimarisha ngome yake ya ushambuliaji baada ya matokeo mabaya katika mechi zao za mwanzo za EPL.

Chelsea mapema kabisa walionesha nia ya kumnasa Pedro lakini kocha Jose Mourinho alionekana kutokua na uhakika.
Kwa sasa  wanarudi katika kinyang'anyiro hicho cha kumnasa mchezaji huyo ambaye ameripotiwa kutokua na furaha Barcelona.

Ushindi wa Man United kufuzu UEFA, van Gaal amwaga sifa kwa Depay

Pia Man City nao walidaiwa kutaka kuingia kwenye sekeseke hili la Pedro, yote kwa yote nafasi kubwa inaonekana kua kwa Man United ambapo Pedro mwenyewe ameonekana kua tayari kuja Old Trafford.
Chelsea nao wanataka kuingilia dili la Pedro?!! Chelsea nao wanataka kuingilia dili la Pedro?!! Reviewed by Steve on Wednesday, August 19, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.