Propellerads

Baada ya kumkosa Pedro, sasa Man United waelekeza nguvu kwa nyota huyu.



Baada ya kuzidiwa kete na Chelsea  katika kumnasa nyota Pedro kutoka
Barca, sasa Man United wameamua kumwinda Sadio Mane wa Southampton.

Winger huyo raia wa Senegal alihamia Southampton akitokea Red Bull Salzburg kwa ada ya £10million na amekua na msimu mzuri tu kwani ameweza kufunga magoli 10.

Nyota huyo aliweka historia pale alipofunga hat trick ndani ya muda mfupi sana katika Premier League (ndani ya dakika 2 na sekunde 56 ) katika mechi ambayo waliwapiga Aston Villa 6-1 mwezi May.

Kwa mujibu wa Telegraph kocha van Gaal amevutiwa sana na mchezaji huyo na inadaiwa tayari ameshamtengea kiasi cha pesa.

Mtendaji wa Manchester United, Ed Woodward alisafiri kuelekea Barcelona Jumatatuu iliyopita ili kukamilisha dili la kumnasa Pedro, lakini kwa sasa inaonekana mshambuliaji huyo yuko mbioni kujiunga na The Blues baada ya kushawishiwa na Cesc Fabregas.

Pedro tayari amesafiri kuelekea London kukamilisha uhamisho wake na Chelsea ambao utagharimu £22m na atakua mchezaji wa nne kusajiliwa na Chelsea majira haya ya joto.
Baada ya kumkosa Pedro, sasa Man United waelekeza nguvu kwa nyota huyu. Baada ya kumkosa Pedro, sasa Man United waelekeza nguvu kwa nyota huyu. Reviewed by Steve on Wednesday, August 19, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.