Propellerads

Hatimaye Pedro asaini rasmi Chelsea, na hiki ndicho alichokisema



Hatimaye klabu ya Chelsea imekamilisha usajili wa aliyekua nyota wa
FC Barcelona, Pedro.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania alitua kwa dau la £21.4million baada ya uvumi wa muda mrefu kua atahamia Manchester United, lakini hali ikawa tofauti na sasa yupo The Blues.

Pedro amesaini mkataba wa miaka minne ambao utambakisha kwa mabingwa hao wa Premier League mpaka mwaka 2019.


Baada ya kutia saini Pedro alisema "Nina furaha sana kua hapa. Nina shauku ya kuonesha maajabu yangu Chelsea na kushinda vikombe.

"Asante kwa klabu na wadau mbali mbali kwa kuniwezesha kuvaa jezi ya blue"

Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa Ujerumani, TZ Online, tayari Chelsea wametoa ofa kwa Bayern na PSG kwa ajili ya nyota wake, Willian ikiwa ni hatua iliyochukuliwa kufuatia ujio wa Pedro.
Hatimaye Pedro asaini rasmi Chelsea, na hiki ndicho alichokisema Hatimaye Pedro asaini rasmi Chelsea, na hiki ndicho alichokisema Reviewed by Steve on Thursday, August 20, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.