Propellerads

Arsenal na Liverpool ngoma ngumu, Cech akiibuka shujaa



Mechi kati ya Arsenal dhidi ya Liverpol imemalizika kwa timu hizo
kutoka sare ya bila kufungana, mechi hiyo ya ligi kuu England ilichezwa kwenye uwanja wa Emirates imemalizika usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne ambapo timu zote zimegawana pointi mojamoja.


Timu zote zilitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini uimara wa walinda milango wa timu zote mbili Petr Cech wa Arsenal na Mignolet wa Liverpool umechangia kwa kiasi kikubwa mchezo huo kumalizika kwa sare tasa.



Coutinho na Benteke walipiga mashuti mengi yaliyolenga lango la Arsenal lakini umaridadi wa Cech aliyesajiliwa Arsenal msimu huu akitokea Chelsea uliisaidia timu ya washika bunduki wa jiji la London kumaliza dakika 90 bila kuruhusu goli.



Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud ameshindwa kutamba kwenye mechi hiyo baada ya kupoteza nafasi kadhaa za wazi zilizotengenezwa na timu yake.


Matokeo hayo yanaifanya Liverpool kufikisha pointi saba na kushika nafasi ya tatu chini ya Manchester City iliyo kileleni kwa pointi tisa ikifuatiwa na Leicester City nafasi ya pili ikiwa na pointi saba  sawa na Liverpool na Manchester United lakini zikitofautiana kwa wastani wa magoli ya kufunga na kufungwa. Arsenal wao wako nafasi ya tisa wakiwa na pointi nne baada ya kucheza mechi tatu pointi sawa na Everton, Norwich na Chelsea lakini nao wakitofautiana kwa wastani wa magoli.


Arsenal na Liverpool ngoma ngumu, Cech akiibuka shujaa Arsenal na Liverpool ngoma ngumu, Cech akiibuka shujaa Reviewed by Steve on Tuesday, August 25, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.