Propellerads

Wakali waliopata kukipiga Man United na Real Madrid kote kote.

Kama tetesi zilizopo sasa zitatimia kweli, Mlinda mlango wa Man United David De Gea na mlinzi wa
Real Madrid Sergio Ramos watahama vilabu vyao na itakua kama wamebadilishana.

Lakini mpaka kufikia mwisho wa usajili mwezi August mambo yatakua wazi kwani uhamisho huu pia unategemea matakwa ya wachezaji wenyewe na ndipo vilabu vitalazimika kuwakubalia.

Leo nakuletea nyota watano waliopata kukipiga kotekote kati ya Real Madrid na Man United.

1: David Beckham




Kama Beckham akiwa mkweli, anaweza akasema angekua na furaha zaidi kama angecheza Man United katika maisha yake yote ya soka, klabu ambayo alichukua nayo makombe sita ya Premier League, makombe mawili ya FA na moja la Champions League, mpaka pale uhusiano wake na sir Alex Ferguson ulipotetereka ambapo ilishuhudiwa akiuzwa Real Madrid kwa dau la pauni mil. 23 mwaka 2003.

SOMA: USAJILI UNAOTARAJIWA KUTISHA ULAYA

2: Michael Owen




Pamoja na kufunga mabao machache lakini muhimu, lakini Man united watamkumbuka mkali huyu kwani wakati wake alikua ni 'unstoppable' kwani aliweza hata kufunga goli dhidi ya mahasimu wao Man City mwaka 2009.
Mwaka 2004 alitua Real Madrid akitokea Liverpool lakini hata ivyo alidumu msimu mmoja tu aliuzwa Newcastle.

3: Ruud Van Nisterlooy




Ni wachezaji wachache sana waliowahi kupata mafanikio katika vilabu vyote viwili, lakini mholanzi huyu aliliweza hilo, akifunga magoli 214 kwa vilabu vyote viwili. Magoli 150 alifunga akiwa na Man United ambayo yaliiwezesha Old Traford kuchukua taji la Premier League, Fa Cup na League Cup, msimu wa 2002/03 aliweza kuchukua Golden Boot ya Premier League.

Kutofautiana na Ferguson kulimfanya auzwe Real Madrid mwaka 2006 kwa dau la pauni mil. 8, akiwa Real Madrid alipata kufunga magoli 41 katika misimu miwili ya mwanzo ambayo yote yaliiwezesha Los blancos kuchukua ubingwa. hata hivyo msimu wake wa mwisho ulitawaliwa na majeraha mpaka alipouzwa Hamburg mwaka 2010.

4: Gabriel Heinze




Wakati akiingia Old Trafford akitokea PSG mwaka 2004 alikua ni kipenzi cha mashabiki wengi wa Man U, hali hii ilipelekea yeye kuchaguliwa mchezaji bora wa klabu katika msimu wake wa mwanzo, msimu wa 2006/07 aliondoka kuelekea Real madrid ambapo alikuemo kwenye kikosi kilichochukua La liga 2007/08, lakini heinze hakuwai kua kikosi cha kwanza Madrid mpaka alipotimkia Marseille mwaka 2009.

SOMA: NYOTA WATANO WALIOKIPIGA ARSENAL NA CHELSEA

5: Cristiano Ronaldo




Huku Van Nisterlooy akiwa na jumla ya magoli 214 akiheshimiwa, Ronaldo yeye kwa hesabu za haraka haraka anayo 431, inashangaza sana!!, Aliingia Old Trafford mwaka 2003 akitokea Sporting lisbon , akiwa na Man United amechukua mataji matatu ya Premier League, FA moja, na Champions League.
Akiwa Los Blancos amechukua kombe moja La liga, mawili ya Copa del Rey na Champions League. Kwa mafanikio binafsi klabuni Real Madrid amepata kuvunja rekodi nyingi na karibia zote zimekuwapo kwa muda mrefu.
Wakali waliopata kukipiga Man United na Real Madrid kote kote. Wakali waliopata kukipiga Man United na Real Madrid kote kote. Reviewed by Steve on Thursday, July 02, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.