Propellerads

Cheki Kiiza alivyotua Airport Dar.

Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Hamis Kiiza ametua jijini Dar es Salaam muda mfupi uliopita kwa ajili ya
kufanyiwa vipimo na kujiunga na mabingwa mara 18 wa Tanzania Babar, Simba.

Kiiza aliyetemwa Yanga Desemba mwaka jana kumpisha mshambuliaji Mliberia Kpah Sherman, ametua jijini hapa akifuatana na kiungo mshambuliaji wa Simba, Mganda mwenzake, Simon Sserunkuma.


Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Rais wa Simba jana, Kiiza atapimwa afya na iwapo akifuzu, atapewa mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo ya Msimbazi.
Cheki Kiiza alivyotua Airport Dar. Cheki  Kiiza alivyotua Airport Dar. Reviewed by Steve on Thursday, July 02, 2015 Rating: 5
Propellerads
Powered by Blogger.