Propellerads

Ushindi wa Simba wasababisha mvutano ndani ya Mbao FC, sasa kipa wao akaliwa kooni




Kitendo cha kipa wa Mbao FC, Erick Ngwengwe, kufungwa mabao 3-2 n Simba katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kumesababishia kukalishwa kitimoto.

Mechi hiyo iliyochezwa Jumatatu wiki hii kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Mbao ilikuwa inaongoza kwa mabao 2-0 ndani ya dakika 45 za kwanza, lakini Simba walisawazisha kipindi cha pili na kuongoza bao la ushindi.

Ofisa Habari wa Mbao, Clisant Malinzi, amesema hawakuridhishwa na mabao aliyofungwa kipa wao na wamemhoji kuhusiana na kipigo hicho.

Malinzi alisema walifungwa na Simba kutokana na kipa wao kuonyesha utovu wa nidhamu ulioigharimu timu kupoteza mchezo huo.

Alisema kutokana na hali hiyo, waliamua kumweka kitimoto kipa huyo kwa lengo la kumhoji na kubaini ana kesi ya kujibu kutokana na kile alichokifanya uwanjani.

"Juzi tulikaa kikao na leo tena uongozi unakutana (jana) na hii inatokana na ukweli kuwa kipa wetu Ngwegwe amegundulika kufanya utovu wa nidhamu uliochangia kuigharimu timu, hivyo anastahili kuadhibiwa.

Suala la adhabu gani atapewa itajulikana kabla ya kucheza mechi yetu inayokuja dhidi ya Tanzania Prisons na itakuwa fundisho kwa wachezaji wengine wenye tabia kama yake," alisema Malinzi.
Ushindi wa Simba wasababisha mvutano ndani ya Mbao FC, sasa kipa wao akaliwa kooni Ushindi wa Simba wasababisha mvutano ndani ya Mbao FC, sasa kipa wao akaliwa kooni Reviewed by Steve on Thursday, April 13, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.