Propellerads

Kuelekea mchezo na Toto, mikakati ya 'ushindi kwa wachezaji ipo namna hii



Baada ya kufanikiwa kupata pointi tatu mbele ya Mbao FC, uongozi wa timu ya Simba umeweka milioni 20 kwa ajili ya kuhakikisha kikosi hicho kinapata ushindi mbele ya Toto Africans kwenye mechi itakayopigwa Jumamosi hii.

Simba itakuwa na kibarua kingine cha kusaka pointi tatu katika Uwanja wa CCM Kirumba mbele ya Toto ambao wamekuwa wakiwasumbua hasa wanapocheza uwanjani hapo na mara ya mwisho Simba kucheza uwanjani hapo waliambulia sare ya bao 1-1.

Mmoja wa mabosi kutoka ndani ya Simba ameweka wazi kuwa fedha hizo ni zile ambazo hutolewa kwa ajili ya bonasi ya kushinda mechi mechi ambapo wameamua kuwasubirisha fedha zao walipoifunga Mbao ambapo sasa watawapa baada ya mechi hiyo na Toto kumalizika.

"Tumetenga milioni 20 kwa ajili ya kuifunga Toto ambayo imekuwa ikitupa shida sana hasa ikicheza hapa kwao na tunaamini kwa jinsi mwenendo wetu ulivyo, ni lazima watupe tu hizo pointi watake wasitake.

"Baada ya mechi na Mbao hatukuwapa wachezaji zile fedha zao za bonasi ya kila baada ya mechi ambapo tumeziunganisha mpaka washinde mechi hii na Toto ndipo tutawapa kwa pamoja ambapo zitakuwa mil 20," alisema bosi huyo.
Kuelekea mchezo na Toto, mikakati ya 'ushindi kwa wachezaji ipo namna hii Kuelekea mchezo na Toto, mikakati ya 'ushindi kwa wachezaji ipo namna hii Reviewed by Steve on Wednesday, April 12, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.