Baada ya Simba, Yanga nao wanataka pointi tatu kutoka mechi na African Lyon, ishu kamili ipo hivi...
Uongozi wa Klabu ya Yanga, umetinga kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya kudai pointi za mchezo wao dhidi ya African Lyon ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.
Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka TFF zinadai malalamiko makubwa ya Yanga ni juu ya mchezaji wa African Lyon, Venance Ludovick, ambaye usajili wake wa kutua hapo akitokea Mbao FC ulikuwa na utata uliosababisha mpaka kufungiwa kuendelea kuitumikia timu hiyo.
Kitendo cha Yanga kudai pointi za mchezo huo, kimekuja siku chacha baada ya Simba kumkatia rufaa beki wa Kagera Sugar, Mohammed Fakhi ambaye inadaiwa alicheza dhidi ya Simba huku akiwa na kadi tatu za njano ambapo ni kinyume na kanuni za ligi hiyo.
Ikumbukwe kuwa, Ijumaa iliyopita, Kamati ya Saa 72 ya TFF ilikutana kujdili masuala mbalimbali yanayohusu matukio y mechi za Ligi Kuu Bara, lakini ilishindwa kutoa majibu ya rufaa hiyo ya Simba huku ikisema inatoa majibu yake kesho Alhamisi.
"Ni kweli Yanga nao wanataka kupewa pointi za mchezo wao dhidi ya African Lyon ambao kama unakumbuka ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 huku bao la African Lyon likifungwa na huyo mchezaji aliyefungiwa, Venance Ludovick.
"lakini mpaka sasa bado majibu yao hawajayapata kutokana na ishu yenyewe kuwepo chini ya kamati ya Katiba na Hadhi za Wachezaji ambayo ndiyo imemsimamisha mchezaji husika, ila nimesikia kamati hiyo inaweza kukutana kesho (leo), kulijadili suala hilo ili majibu ya rufaa ya Simba yakitoka na hii itoke.
"Lakini si Yanga tu ambao wamekuja kulalamika, bali hata wenyewe African Lyon wanahoji ni kwa nini mpaka leo hii mchezaji wao huyo amefungiwa, hivyo wanataka aachiwe huru ili wamtumie kwenye michezo hii ya mwisho kuepuka kushuka daraja," alisema mtoa habari.
Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa alisema ni kweli walikata rufaa juu ya mchezaji huyo tangu ilipomalizika mechi yao na wakatoa Sh laki tatu kwa ajili ya kusikilizwa kwa rufaa yao lakini mpaka leo hakuna majibu yoyote.
Baada ya Simba, Yanga nao wanataka pointi tatu kutoka mechi na African Lyon, ishu kamili ipo hivi...
Reviewed by Steve
on
Wednesday, April 12, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment