Propellerads

Hii kali, Kipa wa Mbao FC adai kuona mauzauza golini mechi na Simba!!



Kipa wa Mbao FC, Erick Ngwengwe, amesema aliona mauzauza kwenye mabao matatu aliyofungwa na Simba, juzi.

Simba ilitoka nyuma na kufanikiwa kushinda kwa mabao 3-2 dhidi ya Mbao ya Mwanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo huo hadi dakika ya 80 Simba walikuwa nyuma kwa mabao 2-0, lakini wakaamka na kufanikiwa kupata ushindi huo uliowapeleka kileleni mwa Ligi Kuu Bara kwa kuwa na pointi 58, mbili mbele ya Yanga wenye pointi 56.

Ngwengwe ambaye kabla ya kufungwa mabao hayo alikuwa ameonyesha kiwango cha hali ya juu, amefunguka kwamba mabao hayo hayakua ya kawaida.

Kipa huyo amesema kuanzia bao la kwanza lililofungwa na Frederic Blagnon hadi la mwisho la Mzamiru Yassin alikua hauoni mpira.

"Kwa namna mabao yalivyokua yanaingia hata watu waliokuwepo uwanjani naamini walikuwa wanashangaa lakini ukweli ni kwamb kulikuwa na mauzauza japo mtu wa kawaida hawezi kuelewa wala kuamini hali ambayo nilikuwa naiona pale uwanjani.

"Kweli nimeumia sana kwa matokeo tuliyoyapata dhidi ya Simba kwani tulikuwa mbele kwa bao 2-0 lakini kipindi cha pili hasa dakika za mwisho nilianza kuona mauzauza kila ninapotaka kushika mpira hata zile bao ukiangalia zimefungwa katika mazingira ambayo mtu wa kawaida huwezi kuamini," alisema Ngwengwe.
Hii kali, Kipa wa Mbao FC adai kuona mauzauza golini mechi na Simba!! Hii kali, Kipa wa Mbao FC adai kuona mauzauza golini mechi na Simba!! Reviewed by Steve on Wednesday, April 12, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.