Propellerads

Majibu ya rufaa ya Simba, pata kujua nje ndani ya kikao cha kamati ya saa 72 kilichotoa maamuzi



Hatimaye timu ya Simba imepewa ushindi wa mezani na Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) kutokana na makosa ya Kagera Sugar kumtumia mchezaji ambaye alikuwa na kadi tatu za njano kitu ambacho ni kinyume cha kanuni ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Uamuzi huo ulitangazwa jana saa tatu kasoro dakika 15 usiku mara baada ya kikao kirefu cha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania maarufu kwa jina la Kamati ya Saa 72 kwenye ofisi za TFF zilizopo Karume jijini Dar es Salaam.

Akitangaza maamuzi ya kikao hicho cha jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Saa 72, Yahaya Mohamed alisema:
"Kamati imepitia rufaa hiyo ya SImba na kujiridhisha kuwa Kagera Sugar ilimtumia mchezaji Mohamed Fakhi kimakosa.

"Kwa mujibu wa kifungu namba 37 Kifungu Kidogo cha Nne cha Kanuni ya Ligi ni kuwa mchezaji atakapofikisha kadi tatu za njano anatakiwa kukosa mchezo unaofuatia ili kufuta kadi alizopata.

"Kikao cha kwanza hakikupata majibu kwa kuwa baadhi ya nyaraka zilikuwa hazijakamilika.

"Imebainika kuwa Fakhi alipata kadi katika mchezo dhidi ya Mbeya City, Majimaji na dhidi ya African Lyon, kwa mujibu wa Kanuni ya 14, Kifungu kidogo cha 37, mchezaji anapotumika akiwa na kadi tatu za njano, timu pinzani inapewa ushindi na mabao matatu.

"Kwa maana hiyo Simba inapewa pointi tatu na mabao matatu katika mchezo huo, maelezo mengine zaidi tutafahamishana," alisema mwenyekiti huyo.

Kutokana na pointi hizo sasa Simba imefikisha pointi 61 na kujitengenezea mazingira mazuri ya kupata ubingwa wakati Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 56.
Majibu ya rufaa ya Simba, pata kujua nje ndani ya kikao cha kamati ya saa 72 kilichotoa maamuzi Majibu ya rufaa ya Simba, pata kujua nje ndani ya kikao cha kamati ya saa 72 kilichotoa maamuzi Reviewed by Steve on Friday, April 14, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.