Sasa ni zamu ya Toto, bado Simba wajigamba kuendeleza dozi Kanda ya Ziwa, Mgosi afunguka haya
Baada ya Simba kufanikiwa kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kuibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Mbao FC juzi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, wameipiga mkwara Toto Africans ambao watakutana nao mwishoni mwa wiki hii.
Kabla ya vinara hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba kuivaa Toto kwenye uwanja huo wa Kirumba, Meneja wa Wekundu hao wa Msimbazi, Mussa Hassan 'Mgosi', alisema wanafanya maandalizi ya kufa mtu ili kunyakua pointi tatu kama kwa Mbao.
Mgosi alisema wanatambua ugumu wa mechi hiyo hasa ukizingatia kwamba timu hiyo ya Toto imekuwa ikihusishwa kuwa na ushirikiano na mahasimu wao, Yanga.
"Sisi tutacheza na Toto kama watahusika na Yanga shauri zao, ila kama tulichowafanya Mbao FC wao wajipange kupata dozi yao," alisema.
Alisema wachezaji wote wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo ambapo kocha Joseph Omog na msaidizi wake, Jackson Mayanja wameendelea kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa Mbao na Kagera Sugar.
"Kikubwa mazoezi yanaendelea vizuri, pia makocha wanarekebisha makosa na kuendelea kuinoa safu ya ushambuliaji ili kuweza kufanya vyema kwenye michezo yetu iliyosalia," alisema Mgosi.
Sasa ni zamu ya Toto, bado Simba wajigamba kuendeleza dozi Kanda ya Ziwa, Mgosi afunguka haya
Reviewed by Steve
on
Thursday, April 13, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment