Huku akihitajika TFF kesho Jumapili, Mkemi hatakwenda kutokana na sababu ambazo mwenyewe ameweka wazi
Siku moja baada ya Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) kumshitaki kwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi, ameibuka na kusema kesho hatofika kusikiliza shitaka lake kwani ana majukumu ya timu yake.
Mkemi alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo kesho Jumapili katika Ofisi za TFF saa 5 asubuhi baada ya kushutumiwa kwa kuidhalilisha Kamati ya Saa 72, kuwa inaendeshwa kwa unazi na imegubikwa na rushwa katika kushughulikia suala la kadi tatu za njano kwa mchezaji wa Kagera Sugar, Mohamed Fakhi.
Akizungumza, Mkemi amesema "Sitaweza kwenda kusikiliza nilichoitiwa katika siku hiyo ya Jumapili kwani nipo Mwanza na timu na ndiyo kiongozi wa msafara.
"Tunacheza na Mbao hiyo Jumapili hivyo nimeandika barua kwa TFF kuwataarifu kuwa sitoweza kufika siku hiyo kama kamati ilivyonitaka hivyo wanipangie siku nyingine.
"Mimi sio mhalifu isipokua ni tuhuma tu juu yangu hivyo nitakapopangiwa siku nyingine nitakwenda na wamekubali ombi langu hilo."
Hata hivyo, alipotafutwa Mtendaji Mkuu wa TPLB, Boniface Wambura simu yake iliita bila kupokelewa.
Huku akihitajika TFF kesho Jumapili, Mkemi hatakwenda kutokana na sababu ambazo mwenyewe ameweka wazi
Reviewed by Steve
on
Saturday, April 29, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment