Propellerads

Rakitic akipa saluti kikosi cha Barcelona jana kilichofanya maajabu mbele ya PSG




Kiungo wa Barcelona, Ivan Rakitic amefunguka kwamba
ni ngumu kuamini maajabu yaliyofanywa na timu yake baada ya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 6-5 dhidi ya Paris Saint-Germain katika hatua ya mwisho ya 16 bora michuano ya klabu bingwa Ulaya.

Wakali hao wa Catalan walikuwa na nafasi finyu ya kusonga mbele hatua ya robo fainali baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa 4-0 ugenini.

Mchezo wa kusisimua uliopigwa jana Jumatano usiku katika dimba la Camp Nou ilionekana ni kama Barca wana ndoto zisizowezekana, hata hivyo bao la Sergi Roberto dakika ya 5 ya nyongeza lilibadilisha kila kitu.

"Siamini, ilikua haiwezekani kabisa. Dakika 15 mpaka 20 za mchezo ilikua ajabu," Rakitic aliiambia BT Sport . "Shukrani ziende kwa timu, kwa klabu na watu wote klabuni na mashabiki. Ilikua ni siku muhimu sana ni ngumu kuelezea chochote.

"Mchezo wa kwanza Paris ulikua mgumu kwetu, watu wengi walisema mengi kuhusu timu yetu lakini yote tuliyapokea. Ni historia. Tunataka kuendelea mbele.

"Tunatakiwa kuamini, 4-0 ilikuwa ngumu, lakini ndio soka. Tuliona kwenye Super Bowl, chochote kinawezekana katika michezo. Leo ilikua ni maajabu, hii ndi Barcelona, klabu bora zaidi ulimwenguni na tunataka kuendelea na ndoto zetu katika klabu bingwa." alisema Rakitic.

Magoli ya Barcelona jana yaliwekwa nyavuni na Suarez (3'), Kurzawa (40' og.), Messi (50' pen.), Neymar akitupia mbili (dakika ya 88', na 91' kwa mkwaju wa penalti), Roberto dakika ya 95' huku bao pekee la PSG likifungwa na Edinson Cavani dakika ya 62. Ambapo matokeo ya jana yakiwa 6-1 huku ya mchezo wa kwanza ikiwa ni 4-0 na kujumlisha matokeo kufikia idadi ya 6-5 hivyo Barca kufanikiwa kuendelea hatua ya robo fainali.
Rakitic akipa saluti kikosi cha Barcelona jana kilichofanya maajabu mbele ya PSG Rakitic akipa saluti kikosi cha Barcelona jana kilichofanya maajabu mbele ya PSG Reviewed by Steve on Thursday, March 09, 2017 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.