Tegete na wenzake waishinda Yanga katika kesi hii
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Jerry Tegete ameipiga kumbo
klabu yake hiyo ya zamani na kutakiwa imlipe kitita chake cha Sh milioni 10.
Taarifa kutoka ndani ya TFF, zimesema Tegete ambaye sasa anakipiga Mwadui inatakiwa alipwe fedha hizo ambazo zinatokana na Yanga kuvunja mkataba wake pamoja na fedha nyingi ambazo ni zake.
“Wameamua nilipwe kwa kuwa ni haki yangu,” alisema Tegete alipohojiwa na blog ya Saleh Jembe.
Pamoja na Tegete wengine waliotakiwa kulipwa ni Omega Seme ambaye pia alikuwa akidai.
Kawaida, klabu nyingi zimekuwa zikiingia kwenye mgogoro na wachezaji kutokana na suala la mikataba na hasa wakati wa kuvunja.
Tegete na wenzake waishinda Yanga katika kesi hii
Reviewed by Steve
on
Sunday, October 09, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, October 09, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment