Propellerads

Baada ya kipigo kutoka kwa Chelsea, Mourinho amegundua makosa kadhaa




Bosi wa Manchester United, Jose Mourinho amechukulia kipigo cha
magoli 4-0 mbele ya Chelsea kua kimetokana na makosa makubwa ya ulinzi.

Magoli kutoka kwa Pedro, Gary Cahill, Eden Hazard na N'Golo Kante yalitosha kumpa kipigo kikubwa kocha huyo Mreno na kikosi chake akiwa katika dimba la Stamford Bridge kwa mara nyingine.

"Tulikua tunaelekea kua na mbinu za kushambulia, tulitaka kutengeneza nafasi, tulilionesha hilo baada ya 1-0," aliiambia Sky Sports News "Goli la pili na la tatu yalikua ni ya kushtukiza.

"Ni miongoni mwa siku tumewafaidisha wapinzani kwa kutofanya lolote. Tulifanya makosa makubwa ya kiufundi, makosa binafsi ambayo yanakugharimu."

Matokeo hayo yamepelekea United kua nafasi ya saba baada ya michezo tisa huku  Chelsea wakipanda mpaka nafasi ya nne.
Baada ya kipigo kutoka kwa Chelsea, Mourinho amegundua makosa kadhaa Baada ya kipigo kutoka kwa Chelsea, Mourinho amegundua makosa kadhaa Reviewed by Steve on Monday, October 24, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.