Propellerads

Uganda wamaliza ukame wa miaka 38 kucheza AFCON, pia kuna matokeo mengine na timu zote zilizofuzu



Uganda 1-0 Comoros

Uganda wamefuzu kucheza michuano ya kombe la mataifa Afrika kwa mara ya kwanza
ndani ya miaka 37, baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Comoro, shukrani zimwendee mshambuliaji Farouk Miya.

Burkina Faso 2-1 Botswana

Burkina Faso nao wamejichukulia tiketi yao kuelekea Gabon, baada ya kushinda kwa 2-1 mbele ya Botswana katika kundi D.

Malawi 1-0 Swaziland

Goli la Gerard Phiri Jr dakika ya 8 lilitosha kuwapatia ushindi wa kuongoza Malawi katika mchezo wao wa mwisho kundi L, hata hivyo timu hizi zote hajijafuzu kucheza Afcon.

Guinea 1-0 Zimbabwe

Zimbabwe wao walimaliza kwa kipigo kutoka kwa Guinea, lakini hata hivyo wao tayari walishafuzu.

Tunisia 4-1 Liberia

Katika kundi A, Tunisia wamefuzu kwa kuwachapa Liberia kwa mabao 4-1.

Togo 5-0 Djibouti

Togo wamefuzu wakiwa ni miongoni mwa vikosi bora kabisa baada ya kuwachapa Togo kwa 5-0 katika mchezo uliopigwa Jumapili jioni.

Algeria 6-0 Lesotho

Algeria wamemaliza mbio za kuelekea Afcon kwa ushindi mkubwa wa 6-0 mbele ya Lesotho Jumapili jioni kwa mabao ya Riyad Mahrez, El Arbu Soudani, Saphir Taider na Ryad Boudebouz.

Timu 16 zilizofuzu:  Gabon, Cameroon, Algeria, Zimbabwe, Tunisia, Togo, DRC, Mali, Burkina Faso, Uganda, Guinea-Bissau, Morocco, Egypt, Ghana, Ivory Coast, Senegal.

Uganda wamaliza ukame wa miaka 38 kucheza AFCON, pia kuna matokeo mengine na timu zote zilizofuzu Uganda wamaliza ukame wa miaka 38 kucheza AFCON, pia kuna matokeo mengine na timu zote zilizofuzu Reviewed by Steve on Monday, September 05, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.