Sanchez alijifananisha na Messi na Ronaldo, Wenger ana mtazamo huu
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kwamba Alexis Sanchez
ana nguvu na uwezo kufikia viwango vya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Mapema wiki hii, Sanchez alidai kwamba ana uwezo sawa kama nyota hao wawili wanaochukuliwa bora ulimwenguni na sasa kocha Wenger amefunguka kwamba Sanchez anatakiwa kuboresha msimamo wake, huku pia akidai ana uwezo wa kufanana na Messi na Ronaldo.
Wenger aliwaambia waandishi "Hicho ndio anachotakiwa kufanya, lakini unajua Ronaldo na Messi wamefanya vile kwa miaka kadhaa kwa hiyo msimamo wa viwango vyao unawaonesha.
"Nina imani Alexis anaweza kua vile. Matamanio yake na pia ni mtu anayetaka kushinda kila mchezo kwa hiyo ni vizuri kua na matamanio kama vile ili kua bora. Ana uwezo wa kua bora, ni yeye mwenyewe tu kuonesha vile."
Sanchez alijifananisha na Messi na Ronaldo, Wenger ana mtazamo huu
Reviewed by Steve
on
Saturday, September 10, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, September 10, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment