Ronaldinho anaamini mrithi wa Messi ni huyu
Mkongwe wa FC Barcelona, Ronaldinho amefichua kuhusu anayemfikiria
atakua mrithi wa Lionel Messi kama mchezaji bora ulimwenguni.
Mkongwe huyo, amekua balozi rasmi wa klabu hiyo ya Catalunya wakati wa ufunguzi wa ofisi zao mpya New York wiki hii.
Huku akisisitiza kwamba Messi ndiye mchezaji bora zaidi kwa sasa, anaamini Neymar anastahili kumrithi nyota Mu-arjentina.
"Kila zama zina mchezaji wake bora. Kila mmoja alikua bora kwa wakati wake. Na Leo ni bora kwa sasa," aliiambia Sport.
"Nadhani Neymar atafikia kiwango cha Leo.
"Anaenda kuwa bora wakati wake. Ni kijana na ameshinda mara nyingi."
Ronaldinho anaamini mrithi wa Messi ni huyu
Reviewed by Steve
on
Saturday, September 10, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Saturday, September 10, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment