Rooney sasa sio chaguo la uhakika kikosi cha kwanza, vipi uamuzi wake? je ataondoka!!
Kapteni wa Manchester United, Wayne Rooney ameripotiwa
kwamba hana mpango wa kuondoka klabuni hapo hivi karibuni na huenda akakaa mpaka angalau kufikia majira ya joto 2018.
Nyota huyo hakupangwa kwenye kikosi kilichoshinda 4-1 kwa Leicester Jumamosi hivyo kuzusha minong'ono kwamba huenda ndio ukawa ndio mwisho wa Rooney.
Mourinho alisisitiza maamuzi hayo yalikua ya kiufundi zaidi ambayo huenda pia yalipelekea ushindi huo.
Kwa mujibu wa Daily Express, Rooney amekubali kwamba kwa sasa hana uhakika wa kupangwa kikosi cha kwanza na yupo tayari kwa hilo huku Mourinho na mchezaji huyo wakiwa na matumaini ya kila mmoja kufanya makubwa.
Rooney anatarajiwa kurejea uwanjani Jumamosi ambapo United itawakaribisha Old Trafford klabu ya Zorya Luhansk kutoka Ukraine katika michuano ya Europa.
Rooney sasa sio chaguo la uhakika kikosi cha kwanza, vipi uamuzi wake? je ataondoka!!
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 27, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Tuesday, September 27, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment