Propellerads

Ronaldo alikasirika kutolewa nje na Zidane, ndani ya chumba cha kubadilishia nguo haya yalijiri




Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameripotiwa
kukwaruzana na meneja wake Real Madrid, Zinedine Zidane katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya kupata sare ya 2-2 mbele ya Las Palmas Jumamosi.

Meneja huyo Mfaransa alimtoa Cristiano Ronaldo wakati Real wakiongoza kwa 2-1 huku zikiwa zimesalia dakika 20 kabla ya mchezo kumalizika.

Ronaldo alionekana kushtushwa na maamuzi ya meneja wake huku akionekana kutoka uwanjani amekasirika.

Kwa mujibu wa Madrid-Barcelona.com, nyota huyo wa zamani wa Man United alimuwakia Zidane kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

"Umenivunja moyo," Ronaldo anadaiwa kumwambia Zidane.

"Tuliza hasira Cris, ulitakiwa kupumzika, utacheza dakika 90 dhidi ya Dortmund ," Zidane alimjibu ktika hali ya kumtuliza hasira.

Kapteni wa klabu, Sergio Ramos pia aliingilia kati "Usiwe hivyo," huku Ronaldo akionekana kwenye kona akiwa ameuchuna bila kumsemesha mtu yeyote.


Ronaldo alikasirika kutolewa nje na Zidane, ndani ya chumba cha kubadilishia nguo haya yalijiri Ronaldo alikasirika kutolewa nje na Zidane, ndani ya chumba cha kubadilishia nguo haya yalijiri Reviewed by Steve on Tuesday, September 27, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.