Propellerads

Kitu kimoja tuu Omog anakazia kwa sasa na Yanga wataisoma




Kocha Joseph Omog amekomalia suala la upotezaji wa
nafasi ambalo limekuwa kubwa katika kikosi chake cha Simba.

Simba imeweka kambi mjini Morogoro, ikifanya maandalizi dhidi ya mechi ya watani wake Yanga, Oktoba Mosi.

Katika mazoezi yake, Omog amekuwa akiwasisitiza wachezaji wake kufunga ikiwezekana kwa asilimia 90 katika nafasi wanazozipata.

Kwani kila wanapofika kwenye eneo la lango, amekuwa akisimamisha mpira na kuwasiistiza namna ya kuzitumia nafasi.

Simba imekuwa ikipoteza mechi zake nyingi za kufunga kila inapokuwa inashambulia katika mechi mbalimbali za ligi inazocheza.
Kitu kimoja tuu Omog anakazia kwa sasa na Yanga wataisoma Kitu kimoja tuu Omog anakazia kwa sasa na Yanga wataisoma Reviewed by Steve on Tuesday, September 27, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.