Propellerads

Di Maria inawezekana akarejea Premier League tena, mara hii inaweza kua klabu hii



Nyota wa Paris Saint-Germain Angel Di Maria huenda
akarejea tena ligi kuu ya England, Premier League.

Nyota huyo Mwarjentina alijiunga na United mwaka 2014 lakini aliondoka mwaka mmoja baadaye akidumu kwa msimu mmoja pekee baada ya mambo kwenda kinyume na matarajio ya wengi.

Kwa mujibu wa Don Balon, kocha wa Chelsea, Antonio Conte anataka kumrejesha tena Di Maria EPL huku mchezaji huyo akionekana kua katika wakati mgumu Ligue 1.

Ripoti zinadai kwamba Di Maria anataka kuwaonesha mashabiki wake na yeye mwenyewe kwamba anaweza kufanya vizuri England lakini sio Chelsea pekee wanamtaka kwani vilabu kadhaa vya Premier League vinamfatilia kwa karibu.

Bosi wa Chelsea Conte anadaiwa kutaka kumsajili Mwarjentina huyo kuongeza nguvu kikosini Stamford Bridge.

Di Maria inawezekana akarejea Premier League tena, mara hii inaweza kua klabu hii Di Maria inawezekana akarejea Premier League tena, mara hii inaweza kua klabu hii Reviewed by Steve on Monday, September 26, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.