Bilionea wa Nigeria kuinunua Arsenal ndani ya kipindi hiki
Bilionea kutoka Nigeria, Aliko Dangote, amedai kwamba
anatarajia kuinunua klabu ya Arsenal ndani ya miaka mitatu au minne ijayo.
Hii sio mara ya kwanza kwa tajiri huyo namba moja Afrika, kwani aliwahi pia kutangaza mpango wake huo mwaka jana.
Dangote ambaye utajiri wake unakisiwa kufikia $ bilioni 10.9 ameathiriwa na kushuka kwa thamani ya pesa ya nchi yake ambapo amepoteza kiasi cha karibia $ bilioni 4.4 mwaka huu.
Hata hivyo, Dangote ambaye biashara zake zinatanuka kwenye sekta ya mafuta, bado anatumaini kununua wakali hao wa Premier League ambao yeye ni shabiki wa damu.
Alipoulizwa katika mahojiano na Bloomberg Television kama anatarajia kuinunua Arsenal, Dangote alijibu "Labda miaka mitatu mpaka minne. Swala ni kwamba tuna changamoto ya kubadilika kwa upepo. Ninataka kujiweka sawa sasa na kua vizuri. Halafu nitakomaa na hili.
"Sio kununua tu Asenal na kuendelea na biashara zingine. Ni kununua Arsenal na kuibadilisha. Ninaendesha biashara zenye mafanikio kwa hiyo ninaweza kuendesha timu yenye mafanikio. Kwa sasa tuna $ bilioni 20 za miradi, kwa hiyo siwezi kufanya vitu vyote viwili."
Bilionea wa Nigeria kuinunua Arsenal ndani ya kipindi hiki
Reviewed by Steve
on
Thursday, September 22, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Thursday, September 22, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment