Propellerads

Bale anataka kuweka historia zaidi



Gareth Bale ameisaidia timu yake kuanza kwa ushindi mbele ya Moldova
katika kampeni ya kufuzu kucheza kombe la dunia 2018.

Kikosi cha Wales kilifikia nusu fainali ya Euro 2016 ikiwa ni mashindano yao makubwa tangu mwaka 1958, na wameendeleza ushindi tena.

Bale amefunga mawili, moja likiwa ni kwa penati, huku Sam Vokes na Joe Allen wakifunga katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Moldova.

"Tunajua hii michezo ni migumu, timu zinakua ngumu," Bale aliiambia Sky Sports News "Tunajifunza zaidi kama timu.

"Nyuma tulifurahia, lakini ishakua historia sasa tunataka kufanya zaidi."

Bale kwa sasa ndiye mfungaji bora wa pili wa muda wote wa Wales akiwa na magoli 24.

Katika michezo mingine ya jana kufuzu kombe la dunia matokeo ni kama ifuatavyo:

Georgia 1-2 Austria

Croatia 1-1 Turkey

Israel 1-3 Italy

Serbia 2-2 Rep. Ireland

Spain 8-0 Liechtenstein

Ukraine 1-1 Iceland

Wales 4-0 Moldova
Bale anataka kuweka historia zaidi Bale anataka kuweka historia zaidi Reviewed by Steve on Tuesday, September 06, 2016 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.