Baada ya kutoswa kikosi cha Guardiola, Yaya Toure aja na maamuzi yake
Mchezaji bora wa mwaka Afrika mara nne, Yaya Toure
aliachwa kwenye kikosi cha klabu bingwa cha Pep Guardiola, sasa imeripotiwa yeye alivyolichukulia swala hilo kwa namna ya kushangaza.
Wakala wake, Dimitri Seluk amemtupia lawama Guardiola kwa kumtosa mteja wake kikosi cha klabu bingwa akidai Toure atasaini mkataba wa mwanzo na klabu nyingine Januari.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Daily Mail, nahodha huyo wa Ivory Coast ameapa kupigania nafasi yake katika kikosi cha Guardiola, hata kama amevunjwa moyo na maamuzi ya Guardiola.
Inadaiwa kua Toure bado hajakata tamaa kuhusu hatma yake City na anataka kumuonesha kocha mambo tofauti.
Baada ya kutoswa kikosi cha Guardiola, Yaya Toure aja na maamuzi yake
Reviewed by Steve
on
Friday, September 09, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Friday, September 09, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment