Pique afunguka kwanini anapendelea zaidi Man United kuliko Man City
Nyota wa FC Barcelona, Gerard Pique amefunguka kwamba anapendelea
zaidi Manchester United kuliko Manchester City pamoja na kwamba kocha wake wa zamani yupo katika klabu hiyo.
Nyota huyo alikipiga na Man United kwa miaka kwa miaka minne, lakini alikua na wakati mgumu kujihakikishia namba kikosi cha kwanza kabla hajanunuliwa na wana Blaugrana mwaka 2008.
Wakati akifanya mahojiano na gazeti la kihispania, Pique aliulizwa kama atakua anawashabikia City kwa sasa baada ya aliyekua kocha wake, Guardiola kushika nafasi ya kufundisha.
"Kati ya Pepp na United, napendelea wengine," beki huyo aliiambia Marca.
"Nimeishi pale vizuri miaka kadhaa iliyopita, na ninapachukulia kama nyumbani kwangu kwingine. daima nitakua Red Devil.
"Ingawa ninaweza kusema napendelea Manchester City kwa sababu kuna watu ninawafahamu pale, kama vile Txiki (Begiristain) aliyenisaidia kuja Barcelona, na wana kikosi wenzangu kama vile (Jesus) Navas na (David) Silva.
"Naipenda Premier League kama shabiki. Ni igi ambayo utaipenda haraka." alimaliza Pique.
Pique afunguka kwanini anapendelea zaidi Man United kuliko Man City
Reviewed by Steve
on
Sunday, August 28, 2016
Rating:
Reviewed by Steve
on
Sunday, August 28, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment