Propellerads

Mourinho kuwaacha Diego Costa,Fabregas, na Ivanovic




Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho anadaiwa kua katika mpango
wa kuwaacha  Diego Costa, Cesc Fabregas na Branislav Ivanovic katika kikosi kitakachoanza dhidi ya Maccabi Tel Aviv kwenye mechi ya ligi ya mabingwa kesho jumatano.

Mabingwa hao watetezi wa Premier League wamekua na mwanzo mbovu katika kutetea taji lao msimu huu huku wakiwa katika nafasi ya 17 kwenye msimamo wa ligi kwa pointi nne pekee kati ya michezo mitano, na wachezaji wengi wanalaumiwa kwa kua na perfomance mbaya.

Kwa mujibu wa gazeti la The Times, kocha huyo Mreno badala yake atawaanzisha  Loic Remy, Oscar na nyota mpya Baba Rahman.

Pia gazeti hilo lilidai kua mmiliki wa klabu  Roman Abramovic bado ana imani kubwa na Jose Mourinho pamoja na matokeo mabovu ya sasa.

Hii ni kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1988 kwa Chelsea kua na matokeo mabovu mwanzoni
mwa ligi.

Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na tuffollow Twitter @Kandanda 24
Mourinho kuwaacha Diego Costa,Fabregas, na Ivanovic Mourinho kuwaacha Diego Costa,Fabregas, na  Ivanovic Reviewed by Steve on Tuesday, September 15, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.