Propellerads

Di Maria afunguka kuhusu Van Gaal na kuondoka kwake Man United



Angel Di Maria amethibitisha kua mahusiano yake yasiyoridhisha
na kocha Louis van Gaal ndio sababu iliyopelekea yeye kuondoka.

Mchezaji huyo wa kimataifa kutoka Arjentina aliondoka Man United na kujiunga PSG msimu huu ikiwa ni baada ya kucheza msimu mmoja pekee.

Di Maria akitokea Real Madrid alianza vizuri kwa kufunga bao dhidi ya Leicester, lakini hata hivyo siku zilivyokua zikikatika ndio mambo yakaanza kua magumu kwake Old Trafford ambapo amethibitisha uhusiano wake mbovu na kocha Van Gaal ndio sababu.

Akiliambia gazeti moja la Ufaransa liitwalo  Le Parisien, Di Maria amesema "Kiukweli, sisi (familia yake) hatukua na furaha, mwanzoni tulikua vizuri kidogo lakini baadae mambo yakawa magumu.

"Sikua vizuri na kocha kwa hiyo nadhani maamuzi ya kuja Paris yalikua ni sahihi.

"Baada ya kutofautiana hakukua na sababu ya kuendelea kukaa.Familia yangu haikua na furaha, mwanangu alipata matatizo, kwa hiyo ilikua ni bora kuondoka."

Ungana nasi kupitia Facebook kwa ku like ukurasa wetu wa Kandanda 24 na tuffollow Twitter @Kandanda 24


Di Maria afunguka kuhusu Van Gaal na kuondoka kwake Man United Di Maria afunguka kuhusu Van Gaal na kuondoka kwake Man United Reviewed by Steve on Monday, September 14, 2015 Rating: 5

No comments:

Propellerads
Powered by Blogger.